Haruna Niyonzima
Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame mwezi
uliopita, Migi (24) alijiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili
akitokea APR ya Rwanda.
Lakini kiungo fundi anayesifika kwa mabao ya kichwa na mashuti ya
kushtukiza huyo angeweza kuwa ni mchezaji wa Yanga sasa kama angefuata
ushawishi wa Niyonzima.
Katika mahojiano na moja vituo vya televisheni vya jijini Dar es
Salaam juzi usiku, Migi alisema: "Niyonzima alinishauri nijiunge na
Yanga (badala ya timu ya Chamazi), lakini uamuzi wangu ulikuwa kujiunga
na Azam.
"Ukiwauliza mashabiki wa 'Apere' (APR) kuhusu safu bora ya kiungo
iliyowahi kutokea kwenye timu yao, watakwambia ile niliyocheza na
Niyonzima. Huyu jamaa ni fundi sana. Ninafurahi kucheza naye kwenye ligi
moja hapa Tanzania.
"Tunaporudi timu ya taifa ya Rwanda, yeye ni nahodha na mimi ni
msaidizi wake. Nilipenda hata kucheza naye timu moja, lakini Azam ni
timu bora ambayo ina kila kitu... Miundombinu ya kisasa pamoja na walimu
wazuri kama klabu za Ulaya."
Kiungo huyo aliyekabidhiwa jezi namba 16 Azam, amewahi kuchezea timu za Kiyovu Sport (2003-2006) na APR (2007 - Julai 14, 2015)
Ameichezea 'Amavubi' mechi 27 na kuifungia bao moja, na katika michezo 102 ya APR amefunga magoli 32.
CHANZO:
NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni