NAMBA NA MAANA ZAKE KIBIBLIA.
Utanguizi.
Tunapoendelea kujifunza maneno ya Mungu, Leo nimepewa fulsa ya
kujadiliana kuhusu Namba ndani ya biblia na maana yake katika maisha
yetu ya kimwili na Kiroho hapa Duniani..Namba ndani ya biblia zimewekwa
na Mungu na tunatakiwa kuziangalia kwa umakini wake sana kama vile
maneno(text) tunavyoyatumia.Tumepewa na Mungu kanuni ya kulinganisha
mambo ya Kiroho na Roho(1Wakoritho 2:13) Na inatuonesha ya kwamba Biblia
na yaliyomo ndani yake ni sehemu ya mambo ya Kiroho.Na tunajua ni
lazima tutafute na kujua kwa namna gani Mungu anazitumia namba. Biblia
ni kitabu sahihi kabisa hakina makosa wote tunafahamu na yamevuviwa na
Mungu (pumzi ya Mungu). Vilevile Namba ni sehemu ya Maneno kwa maana
nyingine tunasema ndani ya maneno kuna namba. Mungu ameweka maneno yake
ndani ya biblia kiasi kwamba hata mtoto mdogo wa miaka 6 anaweza kuelewa
kwa usahihi kabisa kama mtu mzima kama Mungu anavyotaka. Ni kweli
Biblia ni kama msitu unaweza potelea huko na usiweze kuelewa lakini kwa
msaada wa Roho mtakatifu tunaweza kuelewa ukweli wote wa biblia (Mark
4:11-12;Mithali 25:2;1Wakori. 2:11-14).
Jambo la msingi hapa ni lazima uelewe kwanza kwamba Namba ni maneno
(Numbers are words) ndipo utakapo zitumia namba vizuri bila shida kama
maneno.
Sasa kwa nini kwa nini ? Ni kwa ni nadra sana kuona somo hili likifundishwa
Si kwamba namba zote ndani ya biblia zina maana flani ila kwa madhumuni maalum kwa mfano;
1 .Namba zinaweza kutumika katika kupima muda (Kutoka 12:40)
- Namba zinaweza kutumika kuelezea kundi fulani la watu,madhumuni mbalimbali na nk(1petro 3:20).
- Namba zinaweza kutumika kupima kitu Fulani(Mwanzo 6:15).
- Namba zinaweza kutumika kwa maana Fulani na kwa wakati huohuo maana ya Kiroho au Alama Fulani(Yohana 21:11) samaki 153 waliovuliwa hawa ni samaki halisi waliovuliwa lakini Namba 153 pia ina maana maalum Kiroho lakini imejificha sana kwenye uelewa wetu.
- Kwa wakati mwengine namba zinaweza kuwa na maana ya kiroho au alama Fulani yenye kutambulisha kitu Fulani.
Kwa mfano ,Petro alimuuliza Yesu ni mara ngapi mtu akikukosea unaweza kumsamehe hata mara saba?(Mathayo 18:21)
Na yesu akajibu sio mara saba tu lakini hata sabini mara saba. Sasa 70 x
7 = 490 je Yesu alifundisha tusamehe mara 490 halafu tuwache kumsamehe
mtu? Na tunajua Yesu alitufundisha tuwasamehe watu kama yeyey
alivyotusamehe sisi bure, Na tunafahamu ya kwamba Yesu hakusamehe mara
490 pale msalabani.Alipokufa pale msalabani alisamehe watu na dhambi zao
zote bure (Mark 2:5-12;Yohana 8:10-11;Wakolosai 2:13) kwa hiyo 70×7 ina
maana ya Kiroho zaidi kwamba kusamehe hakuna mwisho (completeness
cycle) hata leo Yesu anasamehe ukitubu na kuacha dhambi zako.
- Namba kubwa ugawanjwa vipande vipande (by using factors) vya namba ndogo ili kuona maana yake Kiroho. Mfano 490 = 70 x 7, 153 = 3x3x17. Namba (3) ni kusudio la Mungu ,Namba (17) kuwapeleka mbinguni wale waliookoka wakati wa mwisho.
Namba ndani ya biblia hazipo kwa bahati bahati tu bali zina makusudio
maalumu kuwekwa hapo.Kwa kifupi na tuanze kujadili Namba moja moja ina
maana gani au ishara gani Kiroho.
Namba 1
Hii ni namba ya Mungu. Mungu ni mmoja ni yeye peke yake hakuna Mungu mwingine.
Namba 2
Namba 2 ni Namba ya wale waeneza Neno la Mungu (Wainjilishaji) Kwa
mfano Yesu aliwatuma wanafunzi wake 70 “Wawili wawili”(Luka 10:1).
Ufunuo 11 tunaona wale Mashaidi 2 waliouwawa na baadaye wakafufuka
kutangaza Neno la Mungu. Matendo 13, Paulo na Barnabas walipelekwa
pamoja kama Wamisionari wa kwanza kutangaza neon la Mungu. Kwa hiyo
Namba 2 kama ina maana Kiroho au ina alama fulani basi kwa wale
wasambaza neno la Mungu Wainjilisti na watu wengine waoeneza neon la
Mungu kwa njia moja au nyingine. (Nimefanya utafiti kwa ku angalia miaka
na tarehe ya kuzaliwa na katika maisha yao kwa ujumla namba 2
inajitokeza sana )
Namba 3
Namba 3 Ni Kusudio la Mungu/Kusudi la Mungu kwa
mfano wakati wa tukio zima la kusulubiwa kwa bwana Yesu Lilikuwa ni
kusudio la Mungu mwenyewe.Kumbuka kulikuwa na Misalaba 3(Marko 15:27)
Petro alimkana Bwana Yesu mara 3(Marko 14:66-72) Mitume 3 walikuwa
pamoja na Bwana yesu pale bustani ya gethsemani(marko 14:33),Bwana Yesu
aliomba mara 3 mle Bustanini(marko 14:32-41),Jina “YESU WA NAZARETH
MFALME WA WAYAHUDI” Liliwekwa msalabani kwa lugha 3 (Yohana 19;19-20)
makundi 3 Makuhani, Viongozi wa dini na waalimu na Wote walitaka Yesu
asurubiwe(Mathayo 26:59)nk.Vilevile kuna Namba inaweza kujitokeza katika
namba kubwa lakini zikiwa sawa na 3 kama Yuda alipewa vipande 30
kumsaliti Yesu(Mathayo 26:15), Kulikuwa giza masaa 3 kutoka saa 6 mpaka
saa 9, 12, 27 nk (mathayo 27:45).Kwa matukio yote hayo hii namba 3
inayojirudirudia ni kwa bahati mbaya au ni kwa kusudi maalum? Namba 3
hapa inatuonyesha kwamba tukio lote la kusulubiwa kwa Bwana Yesu ilikuwa
kwa Makusudi ya Mungu (purpose of God/willing of God) Fikilia kukiwa na
mashaidi wawili watatu basi neno lidhibitike, pakiwa na wawili watatu
na Mimi Mungu nipo pamoja nao.
Namba 4
Namba 4 inamaanisha dunia nzima (Ulimwengu) (worldwide) Biblia
inatabua kwamba kuna pande 4 za dunia Mashariki,Magharibi,Kaskazini na
Kusini (zaburi 107:3). Biblia Inazungumzia pepo (winds) 4 za dunia
(Mathayo24:31) na inatambua kuna pande 4 za dunia (Ezk 7:2).Kwa hiyo
kama namba 4 inamaanisha alama yeyote au maana yeyote Kiroho basi
inatambulisha Dunia au Ulimwengu kwa ujumla.
Vilevile namba 4 iamaanisha ukamilifu wa jambo linapofikia mwisho kabisa
(hitimisho la jambo) kwa mfanoYesu alisubili mpaka siku 4 Lazaro
alipokufa kabla yakufufuliwa (Yohana 1:15-17) Mfalme Jehu’aliruhusiwa
kutawala kizazi cha 4 (2Wafalme 10:30,13:1,9-10,14:16,2915:8-18) Israeli
walikaa utumwani mpaka kizazi cha 4 baada ya kutumikishwa miaka zaidi
400 (Mwanzo15:13-16).Abraham alinunua kipande cha ardhi kwa ajiri ya
kumzikia Sarah mkewe kwa shekeli 400 (Mwanzo23:15) Kwa hiyo kwa maaana
hii Namba 4 vivile ina maana ya utimilifu wa kitu au mwisho wa kitu ktk
muda, kwa kipidi Fulani. hata kumaanisha Mwisho wa dunia (2Petro 3:10).
Namba 5
Namba 5 ina maanisha Wokovu au Hukumu.Yesu
alipata hukumu ili tupate Wokovu kwa hiyo usishagae namba 5
ikiwakilisha Wokovu au hukumu kwa wakati mmoja .Namba 5 inaonekana ½.
Namba ya 10, 5 inawekuwa kama 5 50 500 5000 nk. Unaweza kufikiria ushuru
wa hekalu ulikuwa shekeli 5(kutoka 30:13) au wale watu 5000
aliowalishwa chakula Bwana Yesu (Yohana 6:10-13) au unawea kufikiria
wale wanawali 5 wapumbavu na 5 wenye busara (mathayo 25:1-2) nk .kwa
hiyo kama namba 5 ni alama au maana fulani ya Kiroho basi ni hiyo
yaWokovu au Hukumu.
Namba 6
Kama namba 6 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi itakuwa inamaanisha KAZI.
Mungu alitumia siku 6 kuumba ulimwengu (kutoka 20:11).Namba 666 katika
Ufunuo 13:18 ni Wasiookolewa walio kwenye mikono ya shetani wakijitahidi
kupata haki mbele ya Mungu.
Namaba 7
Namba 7 inatumika sana kwenye biblia katika maana ya Ukamilifu wa Ki Mungu (Completed
cycle) (siku7, miaka7) kama kusamehe ni 70x7times maana yake kusamehe
hakuna mwisho samehe samehe samehe……Vile vile namba hii 7 inatabulika
kama na namba ya Mungu. Ukiomba kitu chochote katka Mungu mara 7 hakika
Mungu atakupa jibu.(Tatizo letu tunamchagulia Mungu majibu, Majibu
mengine hatutaki na tunaendelea kuomba kwa hasara).Kwa mfano Ukuta wa
babeli ulidondoka baada waisrael kusunguka mara 6 na mara 7 ukuta
kukadondoka.Naamani aliambiwa akajichofye mara saba na baada ya hapo
ukoma ukapona kabisa.
Namba 8
Namba 8 ni 2×4 au 2x2x2 maana yake ni mchanganyiko wa maana ya namba 2 na namba 4.
Namba 9
Namba 9 ni 3×3.kwa hiyo maana yake ni sawa na namba 3
Namba 10
Namba 10 ni sawa na namba 1inaweza kuwa 10, 100, 1000, 10000…. Nk. Namba 10 ina maanisha Ukamilifu kamili.
Biblia inasema kuhusu sarafu 10(luka 15:8), Kondoo 100 (luka 15:4)
miaka 1,000 (2Petro 3:8),Vizazi 1000 (Kumb.7:9)etc.kwa hiyo kama namba
10 ni alama ya jambo fulani au ina maana fulani kiroho basi ni
Ukamilifu.
Namba 11
Namba 11 inatumika katika biblia inamaanisha mapungufu katika usahihihi (defective
fullness). Kwa mfano kulikuwa na makabila 12 (lakini halisi ni 13) ya
waisraeli, lakini Daudi alipofanya sensa Mungu alisungumzia Makabila
11(1wafalme 11:31-32).Wakati Yuda aliyekuwa mmoja kati ya Wanafunzi wa
Yesu 12 (Yohana 6:70-71) alijiua baada ya kumsaliti Yesu, Walibakia
Wanafunzi 11, Baadaye alichaguliwa Mtume mwingine kuchukua nafasi yake
na kuwa 12 tena.(Matendao 1-13-26). Kwa hiyo namba 11 kama ina alama
yeyote au maana yeyote kibblia basi ni Usaliti.
Namba 12
Kama namba 12 ni alama au ina maana yeyote kiroho basi ni Utimilifu katika muonekano Kwa
mfano kulikuwa na Makabila 12 na Mitume 12, Mji mtakatifu una urefu wa
12000 mara 12000 mara 12000 (Ufunuo 21-16)nk. Kwa hiyo kama namba 12 ina
maanisha alama au ina maana Kiroho basi ni Utimilifu katika
muonekano.Namba 7,10,12 zote zinafanana kila moja kama utimilifu wa
kiroho isipokuwa ikiambatanishwa na namba zingine kama 2×6,2x2x3 nk..
Namba 13
Namaba 13 kama ina maanisha alama au maana fulani ya Kiroho basi ni Hakika ya Utimilifu.
Biblia inasungumzia Mitume 12, Lakini hakika kabisa ni 13. Wa 13 ni
Mtume Paulo aliposisitiza akiwa katika katika roho Mtakatifu kuwa
amekidhi matakwa/Vigezo vyote vya kuwa Mtume kama wale
12.(1Wakoritho9:2;15:8-9; 2Wakoritho12:11-12) Biblia kwa kawaida kabisa
inasungumzia Makabila 12 ya Israel lakini Uhakika na kimsingi Yalikuwa
Makabila 13(Mwanzo 49:1-28;Hesabu 32:33;Joshua 16 na Joshua 17) Namba 13
ina maanisha Uhakika wa Ukamilifu.
Namba 17
Inaonekana sehemu nyingi katika biblia ikisimama kwa maaana ya Mbingu/uungu (Heaven) Kwa
mfano katika miaka 17 ya mwisho ya maisha yake Yakobo chini ya Yusufu
ambaye ni mtoto wake kipenzi ambaye alisalitiwa kama alivyosalitiwa Yesu
wakati alipotumika badala ya Mungu kuwaokoa na njaa kali (Mwanzo
47:28)Yeremia alininunua shekeli 17 kuwanunulia wana wa israel kipande
cha ardhi kuonyesha kwamba Mungu amewarudisha tena kwenye nchi
yao.Kipande kile kilikuwa kinamaanisha Ufalme wa Mungu umewarudia tena
(yeremia 32:9) Kwa hiyo namba 17 kama ina alama au maana ya Kiroho ni
mbingu/ Uungu (heaven).
Namba 37
Kama ilivyo namba 23 zinamaanisha Hukumu ya Mungu.Nuhu
alikuwa kwenye Safina kwa muda wa siku 370 wakati mungu alipo hukumu
dunia(Mwanzo 7:11;8:14-18).Jehsi la Sennacherib liliangamizwa na Mungu
kwa usiku mmoja watu 185,000(2Wafalme 19:35) 185,000 = 5x37x1,000.Namba
666, ambayo ni namba inamaanisha watu wasiookoka wali chini ya hukumu ya
Mungu(Ufunuo 13:18) kama namba hiyo ukiivunja vunja katika namba
ndogondogo ni 3x6x37.Kwa hiyo Namba 37 kama ina alama au maana yeyote
Kiroho basi ni Hukumu..
Namba 40
Namba 40 inajirudiarudia katika biblia ikimaanisha Mwisho wa majaribu/Majaribu.Musa
alikaa siku 40 katika Mlima Sinai(Kutoka 24:18), Huku nyuma Wana wa
Islael walijaribiwa na kushindwa kuvumilia na kutengeneza miungu
yao(Kutoka 32:1-4).Israel walikuwa Jangwani kwa kipindi cha miaka 40
walishindwa na hakuna aliyeokolewa wote hawakufika Kanani isipokuwa
watoto wao amabao waliozaliwa baada ya kutoka Misri.(Waebrania
3:17).Yesu alijaribiwa na shetani siku 40 mchana na usiku (Mathayo
4-1-2:Luka 4:1-2) pamoja na majaribu hayo tunamshukuru Mungu kwamba Yesu
hakushindwa alimshinda shetani (Mathayo 4:3-11;Luka 4-3-14) Kwa hiyo
kama namba 40 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi ni Majaribu.
Fikiria watu wengi wakifikia umri wa miaka 40 shida na masumbufu huwa
yanakwisha na hili kila mtu anaweza kujichunguza au kuchunguza hata kama
maisha ya mtu huyo ni ya kimasikini lakini amani na utulivu unakuwepo
katika maisha yake( Focus on Future destenity) Utu uzima ni miaka 40.
Chunguza 40 zinavyotumika katika maisha na kwa jamii kwa ujumla hizo ni
maana za kiroho kumbuka!
Namba 43
Namba 43 ina maana ya Hukumu au Wokovu.Kwa
mfano Israel walikaa Misri kwa miaka 430.Mwisho wa miaka hiyo 430
hHukumu ilishuka kwa Wamisri na Uhuru Wokovu kwa kwa Israel). Kwa hiyo
namba 43 kama inamanisha alama au maana Kiroho basi ni Hukumu au Wokovu.
Ndugu mpendwa Mungu akubariki na tilia maanani somo hili litakusaidia na
wakati mwingine kukuonyesha njia. Unaweza patwa na shida au jambo
Kumbuka Mungu anazungumza kupitia Namba. Kwa nini 3 kwa nini 7,2,5,10
nk..Mungu anapozungumza na wewe anaweza kukuonyesha ishara mbalimbali za
namba kati jambo fulani katika maisha yako kiroho. Vilevile kumbuka si
kila namba ina maana ya kiroho.
Kuna baadhi ya dini na madhehebu huwa wana utaratibu wa kuhesabu hesabu
vitu Fulani kama ushanga na nk hata kwa wachawi na waganga huwa
wanahesabu hesabu kwa namna Fulani ili kupata namba na maana zake kwenye
mambo yao ya kichawi. Nimekwambia hayo ili uweze kujua kwamba katika
namba kuna siri kubwa kiroho kwetu sisi tulio okoka na kwa wale wasio
mwamini Bwana Yesu.
Asante Mungu akubariki tuombeane
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni