Naibu Waziri Ofisi Ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo, amewatoa hofu
wahitimu wa Kozi ya Ualimu ambao wamekuwa wakisubiri ajira kwa muda
mrefu.
Akizungumza na mtembezi.com leo
Jijini Dsm Naibu Waziri Jafo amewataka wahitimu hao kuwa na subira
kwani ajira hizo zitatangazwa muda wowote kutoka hivi sasa, huku
akiwahakikishia kuwa wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu
wamejipanga kuhakiki idadi ya walimu wanaohitajika.
Ameongeza kuwa licha ya uhakiki huo pia
wizara yake inamalizia takwimu za walimu waliostaafu kazi pamoja na
waliohama kutoka shule binafsi ili serikali iweze kujua idadi halisi ya
nafasi zinazoitajika.
Jafo ameiambia Mtembezi kuwa mwaka huu
serikali inampango wa kuongeza idadi ya ajira za Walimu hadi kufikia
Walimu 40,000 katika ngazi za Shule za Msingi na Sekondari.
Kuhusu ajira hizo Jafo, amefafanua kuwa
mikoa ya Kigoma, Mara, Tabora na Rukwa ndio itapewa kipaumbele kwani
ndio inaongoza kwa kuwa na idadi ndogo ya Walimu na hii itapunguza
kasumba ya wahitimu kozi ya ualimu kupenda kuajiriwa mjini.
Jiunge na http//mbawalastationary.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni