(a) Roho Mtakatifu ni nani?
Roho mtakatifu ni Mungu. Unaposoma katika Neno Mungu unapata
kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu;
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na
kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. (Matendo 5:3-5)
Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. (Matendo 5:3-5)
Petro anaanza na kusema kuwa Anania amemwambia uongo Roho Mtakatifu,
halafu anaishia na kusema kuwa alimwambia uongo Mungu. Maana yake kumwambia
uongo Roho mtakatifu ni kumwambia uongo Mungu.
Maandiko yanasema pia kuwa Muaqngu ni Roho na kwamba wamwabuduo imewapasa
kumwabudu katika Roho na kweli
(b) Makao ya Roho mtakatifu ni wapi?
Roho Mtakatifu hukaa ndani ya kila mtu aliyempokea Kristo
kuwa Mwokozi wake. Maana yake ni kwamba unapookoka ndipo Roho Mtakatifu
anaingia kwako na anaendelea kuishi ndani yako maadamu hali yako inaendelea
kumruhusu akae ndani yako. Neno linatuambia kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani
yetu na kuwa sisi ni hekalu la Mungu na kwamba tunapaswa kuwa watakatifu.
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la
Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa
ndani yenu? … Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo
ndilo ninyi (1Wakorintho 3:16-17).
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la
Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe (1Wakoritho 6:19).
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali
mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si
wake. Na Kristo akiwa
ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa
sababu ya haki.
Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua
Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika
wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu (Warumi 8:9-11).
Siku ile ya
Pentekoste, Neno linatuambia kuwa watu walijazwa Roho Mtakatifu. Kitu hujazwa
ndani ya kitu kingine na si vinginevyo; kwa jinsi hii Roho Mtakatifu aliingia
na kujaa ndani ya watu.
Hata ilipotimia siku ya Pentekoste
walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja
ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza
nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama
ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu,
wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka (Mdo
2:1-4).
(c) Kazi za Roho Mtakatifu
Kazi za Roho Mtakatifu zinaweza kugawanywa katika sehemu kuu
mbili:
(i)
Kazi katika maisha ya mkristo binafsi
(ii)
Kazi kwa ajili ya utumishi
I.
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Maisha ya Mkristo
binafsi
Roho Mtakatifu huingia kuishi ndani ya Mkristo na kumhudumia
binafsi kwa namna mbalimbali:
1. Roho Mtakatifu ni Kiongozi
Kiongozi ni mtangulizi au aliyetangulia kuonyesha njia
sahihi. Wana wa Mungu wanaongozwa na Roho wa Mungu.
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na
Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. (Rumi 8:14). Wale waufuatao
mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake (Rumi
8:8-9).
Haiwezekani kuwa
mwana wa Mungu kama hukuongozwa na Roho wa Mungu. Maana yake ni kwamba ili uwe
mwana wa Mungu ni lazima ukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu. Kuwa Mwana ni
kuwa na haki zote mbele za baba. Mwana ndiye mrithi wa mali za baba yake. Haiwezekani
kuurithi uzima wa milele mpaka umekuwa mwana wa Mungu na huwezi kuwa mwana wa
Mungu mpaka umeongozwa na Roho Mtakatifu.
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri
lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha
habari yake (Yohana 16:13). Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya
sheria (Wagalatia 5:18).
Roho Mtakatifu
ndiye wa kutuongoza na kututia kwenye kweli yote. Ili kumpendeza Mungu ni
lazima kuongozwa na Roho Mtakatikfu akaaye ndani ya mwamini. Kumfuata Roho
Mtakatifu kunasaidia kumpendeza Mungu na wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza
Mungu.
2. Roho Mtakatifu ni Mwalimu
Mwalimu ni yule anayefanya kazi ya kufundisha. Kufundisha ni
kuelekeza au kutoa maarifa aliyonayo mtu kwenda kwa mwingine na kisasa zaidi ni
kumwezesha mtu aweze kujifunza au kupata maarifa mengine zaidi ya yale
aliyonayo na kwa hiyo kuweza kufanya au kusema na kuwaza yale yanayotakiwa. Roho
Mtakatifu anatuwezesha kujua zaidi habari za Mungu na zaidi kujua mapenzi ya
Baba yetu.
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho
Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. (Yohana 14:26).
Na
watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka,
msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa
kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha
saa ile ile yawapasayo kuyasema
(Luka 12:11-12)
Roho Mtakatifu ni mwalimu
aneyetufundisha yote kuhusiana na maisha ya kila siku ya kimwili na kiroho.
Mkristo yeyote asiyejua mapenzi ya Mungu huyo kunakuwa na mashaka kuwa ana Roho
Mtakatifu na kama anaye, basi ni mwanafunzi mbaya asiyezingatia yale
anayofundishwa. Kibaya zaidi ni kwamba ikitokea Mwanafunzi huyu hawezi kufuata
mafundisho ya Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu humwacha. Matokeo ya kuachwa na
Roho Mtakatifu ni kubaki huelewi chochote katika maisha yako kiroho na kimwili-
unaaendelea kubaki mjinga siku zote jambo ambalo ni hatari. Kuwa mwanafunzi
mzuri kwa Roho Mtakatifu. Jambo la kujiuliza hapa ni; Je, unaye huyo mwalimu
maishani mwako? Je, unamsikiliza, kumwelewa na kumtii mwalimu huyo?
3. Roho Mtakatifu Hushuhudia Uhusiano Wa Mkristo Na Mungu
Uhusiano wa Mkristo na Mungu hushuhudiwa na Roho Mtakatifu.
Kwa njia ya Roho Mtakatifu Mkristo hutambua uhusiano wake na Mungu ulivyo,
kwamba ni mzuri au ni mbaya – kwamba
unaye Mungu au hunaye. Kwa sababu hiyo hakuna mtu anayeweza kijitetea
kuwa hajui uhusiano alionao na Mungu wake.
Roho
mwenyewe hushuhudia pamoja na roho
zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu
(Rumi 8:16).
Anayetutambulisha sisi kuwa tu
watoto wa Mungu ni Roho Mtakatifu. Tunaweza kutambua kuwa tumeokoka kwa
kushuhudiwa na Roho Mtakatifu na pia kwamba hatujaokoka, Roho Mtakatifu ndiye
anayetushudia nafsini mwetu.
Yesu Kristo alisema mtu yeeyote
akikaa nadani yake naye atakaa ndani yake lakini kwa sharti moja la kuzishika
amri zake. Tunaweza kujua uhusiano huo pale tu roho Mtakatifu atakapokuwa
ametushuhudia.
Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na
katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa
(1Yohana 3:24).
Katika
yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho (Waefeso
2:22)
Kujua kuwa Yesu anakaa ndani yetu nasi
tunakaa ndani yake ni kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetupa.
Neno la mungu pia linatuambia kuwa
hakuna mtu yeyote aliyemwona mungu wakati wowote isipokuwa tu kama tukipendana.
Hii ni kwa sababu ametushirikisha Roho Mtakatifu.
Hakuna
mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na
pendo lake limekamilika ndani yetu. Katika hili tunafahamu ya kuwa
tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake (Yoh.4:12-13).
Kwa kutushirikisha Roho Mtakatifu,
tunafahamu kuwa tunakaa ndani yake (Yesu) na yeye ndani yetu. Tunafahamu
kukamilika au kutokamilika kwa pendo lake kwetu kwa kushirikishwa na Roho
Mtakatifu. Urafiki wetu na Mungu ni kwa kutii sheria ya Mungu
sawasawa na nia ya Roho ambayo ni uzima na amani.
Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya
Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza
Mungu (Warumi 8:6-8).
Roho Mtakatifu ndiye anayeshuhudia
uhusiano tulionao na Mungu wetu, kwamba ni mzuri au ni mbaya. Kuwa mwangalifu
pale atakapokushuhudia na uwe mtii na kubadilika inapotokea anakujulisha kuwa
mahusiano yako na Mungu si mazuri.
Roho Mtakatifu anatusaidia kuelewa
wokovu halisi ndani yetu. Kwa kutuhakikishia dhambi, haki na hukumu.
Lakini
mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi
nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu,
nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari
ya dhambi, na haki, na hukumu (Yohana 16:7-8).
Ili tuweze kuuona ufalme wa Mungu
ni lazima kuzaliwa (kubatizwa) katika Roho. Mahusiano mazuri na Mungu ndiyo
yatakayotuwezesha kuurithi ufalme wa Mungu na hayawezi kuwepo kama hatukuwa na
Roho Mtakatifu.
Nikodemo
akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye
mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu
asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho (Yohana
3:4-6).
Matendo yetu hayawezi kututhibitishia
uhusiano wetu na Mungu pamoja na haki tulizonazo isipokuwa kwa rehema zake
Mungu na kwa kufanywa upya na Roho Mtakatifu.
si
kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa
kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya
Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa
warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu (Tito 3:5-7)
4. Husaidia Kuishi Maisha ya Kumpendeza Mungu
Ni vigumu sana kuishi maisha ya
kumpendeza Mungu kama tusipoenenda kwa Roho. Miili yetu imejaa tamaa nyingi na
husukumwa kuzitimiza. Hakuna njia ya kuzikwepa isipokuwa tu kwa msaada wa Roho
Mtakatifu.
Basi nasema, Enendeni kwa Roho,
wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani
ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana,
hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi
matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka,
uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo,
katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu
watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini
tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao
walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa
zake. Tukiishi kwa Roho, na
tuenende kwa Roho (Wagalatia
5: 16-25).
Kwa sababu sheria ya Roho wa
uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha
huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti (Warumi 8:2).
Tunamjua Mungu kwa njia ya hekima itokanayo na Roho ya hekima
na ufunuo wa namna ya kumjua yeye.
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya
hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; (Waefeso 1:17).
Roho Mtakatifu ndiye athibitishaye imani yetu kwa Mungu
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia ule la kweli, habari njema za
wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho ule wa
ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi
wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake (Waefeso 1:13-14)
5. Husaidia Katika Maombi
Hufika wakati ambapo wakristo hushindwa kuomba kwa jinsi
iwapasavyo na kwa kiwango ambacho Mungu anaweza kujibu. Wakati mwingine hawajui
kiwapasacho kuomba kwa sababu pia hawajui haja halisi walizonazo katika maisha
yao. Wakati mwingine wakristo huwa na mzigo mzito ambao huwafanya hata
washindwe kuomba kwa sababu ya kulemewa nao. Inapofika nyakati za namna hiyo,
Roho Mtakatifu huingilia kati na kuomba kwa niaba yao. Biblia inasema, Roho
Mtakatifu huomba akituaidia udhaifu
wetu. Na kwamba huomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Kadhalika Roho naye hutusaidia
udhaifu wetu, kwa maana hatujui
kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa
kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo
Mungu (Warumi 8:26-27).
6. Hutoa Nguvu na Uzima wa Miili
Ufufuo wa Yesu una faida sana kwetu. Kitendo cha Yesu
kufufuka kimetusaidia sisi pia kuwa hai katika miili yetu kwa iliyokuwa katika
hali ya kufa. Roho Mtakatifu ndiye aliyemfufua Yesu Roho huyohuyo anakaa ndani
yetu
Lakini,
ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye
aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali
ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu (Warumi 8:11).
II.
Kazi Ya Roho Mtakatifu Kwa Ajili Ya Utumishi
Pamoja na faida za mwamini binafsi ambazo tumeziona kwa kule
kujazwa na Roho Mtakatifu, Mungu pia
anataka kumjaza na kumbatiza mwamini kwa Roho Mtakatifu ili kumtia nguvu za
kumtumikia na kumtukuza Mungu duniani. Bila kuwa na nguvu za ki-Mungu ambazo
tunazipokea kupitia Roho wake Mtakatifu hatuwezi kumtumikia Mungu ipasavyo.
Ndiyo maana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wakae Yerusalemu mpaka hapo wakapokuwa
wamebatizwa kwa Roho Mtakatifu – atakapowaletea msaidizi kwa ajili ya kazi ya
Mungu.
Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali
waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana
alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku
hizi chache (Matendo 1:4-5).
1. Kutoa nguvu na ujasiri wa kushuhudia
Nguvu (uwezo wa kufanya kazi au jambo) na ujasiri (kutenda
jambo bila kuogopa/bila woga/bila mashaka) wa kuweza kumshuhudia Yesu Kristo
unatokana na nguvu ya Mungu iliyoko ndani yako. Nguvu ya Mungu ni uwezo wa
ki-Mungu wa kufanya kazi au jambo. Roho Mtakatifu anapoingia ndani ya mwamini
husababisha mtu huyo kupata nguvu ya Mungu na kupata ujasiri wa kuweza
kushuhudia matendo makuu ya Mungu na habari ya Yesu Kristo kwa ujmla wake. Yesu
Kristo alikaa na wanafunzi wake kwa miaka mingi akiwafundisha na alipomaliza
kazi yake anasema hawawezi kuifanya kazi yake mpaka hapo watakpokuwa wamejazwa
na nguvu za Roho Mtakatifu. Alijua kuwa haiwezekani kuwa mashahidi wake bila
kuwezeshwa na nguvu ya Roho Mtakatifu.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi
mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria,
na hata mwisho wa nchi (Matendo 1:8).
Kwa maneno haya ni dhahiri kuwa mtu hawezi kuwa shahidi wa Kristo
mpaka ajiliwe na Roho Mtakatifu.
Hata
walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote
wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri (matendo 4:31).
Kumbuka jinsi ambavyo Petro alitaka kumfuata Yesu na
kushiriki mateso yake. Petro alimwambia Yesu kuwa atakuwa naye popote
atakapokwenda hata kuteswa, kifo na hata kifungoni.
Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani
au hata kifoni.
Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu
ya kuwa hunijui
…… Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye
Petro akaketi kati yao. Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema,
Na huyu alikuwa pamoja naye. Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. Baadaye kitambo mtu mwingine alimwona
akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi. (Luka
22:33-34, 55-58).
Kanachosababisha Petro amkane Yesu
ni kukosa nguvu na ujasiri wa kumshuhudia Yesu kwa kuwa hana Roho Mtakatifu.
Petro huyohuyo anapojazwa na nguvu za Roho Mtakatifu siku ile ya Pentekoste
anakuwa nguvu na ujasiri wa kuzinena siri za kristo bila kuogopa.
13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja,
akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao
Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya
mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa
kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto …….. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. (Matendo 2:14-41).
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto …….. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. (Matendo 2:14-41).
Yote haya yalifanyika kwa sababu yalijazwa na Roho
Mtakatifu. Aliowaogopa siku ile ya mateso ya Yesu ndio haohao aliowahubiria
siku ya Pentekoste na wakapata kuokoka watu wengi sana.
2. Kuleta ufahamu Mpya wa Neno la Mungu
Ufahamu ni uwezo
wa kuelewa maneno au mambo. Roho Mtakatifu hutusaidia kuyaelewa maandiko
matakatifu yaani Neno la Mungu. Kati ya mambo magumu na mabaya ni kutolielewa
Neno la Mungu ambako husababisha matatizo makubwa.
9 lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio
halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu
aliwaandalia wampendao. 10 Lakini Mungu ametufunulia
sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu
ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna
ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 12 Lakini sisi
hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate
kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 13 Nayo twayanena, si
kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na
Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni (1Wakorintho
2:9-13).
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye
kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote
atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake (Yohana
16:13).
3. Huwezesha kufanya ibada ya kweli ya Mungu
Ibada ni tendo la kuaabudu au sala ya kumwabudu Mungu.
Kufanya ibada takatifu naya kweli huwezekana tu ikiwa tunaye Roho Mtakatifu.
Ibada ya kweli hufanyika ndani ya moyo na haiwezi kufanyika ndani ya Moyo kama
hakuwemo humo Roho Mtakatifu.
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku
mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 20 na
kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu
Kristo; 21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo
(Waefeso 5:18- 21).
4. Kumtukuza Yesu Kristo
Yesu mwenyewe alisema kuwa atakapokuja Roho Mtakatifu
atamtukuza yeye kwa sababu atayachukua yaliyo yake (Yesu) na kutupasha habari.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye
kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote
atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo
yangu na kuwapasha habari. 15 Na yote aliyo nayo Baba
ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na
kuwapasheni habari (Yohana 16:13-15
5. Kushuhudia uhai wa Yesu
Kati ya mambo ambayo ni ya muhimu na ya msingi ni kwa Yesu
kuwa hai. Kama Yesu asingalikufa na kufufuka basi ingalikuwa ni kazi bure kwetu
kuwa Wkristo kwa sababu Wokovu ungalikuwa haupo. Hivyo Roho Mtakatifu ndiye
anayetushuhudia kuwa Yesu yu hai.
30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye
ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. 31 Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa
mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa
dhambi. 32 Na sisi tu mashahidi wa
mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio (Matendo 5:30-32).
6. Kuleta karama za Roho Mtakatifu
Katika kamusi ya
Kiswahili Sanifu neno ‘Karama’ limetafsiriwa kama “Kipawa anachokuwa nacho mtu kwa sababu ya kumwabudu sana Mungu aghalabu
humpa uwezo wa kuomba haja kwa Mwenyezi Mungu na kukubaliwa mara moja; ikibali
ya kupokewa haja iombwayo” na neno ‘kipawa’ linatafsiriwa kama “uwezo mtu aliozaliwa nao ambao humwezesha
kufanya jambo Fulani vizuri”.
Katika kamusi ya
kiswahili kwa kiingereza, neno ‘karama’ limetafsiriwa kama gracious gifts likiwa na maana ya zawadi za neema, ‘Neema’ ni kustahilishwa bila kustahili au bure.
Kwa hiyo zawadi za neema ni zawadi ambazo mtu anazipata bila kustahili au
kuzigharimia. Maana yake mtu anapata zawadi kwa sababu aliyempa ameamua kumpa
na kwamba anaweza kunyimwa yeye na akapewa mwingine na hawezi kudai kwa sababu
siyo haki yake.
Kwa jinsi hiyo
basi karama za Roho Mtakatifu ni zawadi ambazo Roho Mtakatifu huwapa watu
(wakristo wamwabuduo sana) kwa neema na ndiye huamua ampe nani, zawadi gani
bila kujali anapenda au hapendi.
4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. ….. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine
neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine
imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule
mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine
unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine
tafsiri za lugha; 11 lakini kazi hizi zote huzitenda
Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye
(1Wakorintho 12:4, 8-10). Soma pia Matendo 2:4; 10:46 ;19:6
Roho Mtakatifu huzileta karama hizo katika kanisa kwa ajili
ya kurahisisha ujenzi wa kanisa lake pamoja na kazi zake. Ili kanisa lijengeke,
tunahitaji karama mbalimbali za Roho Mtakatifu. Karama zipo tofautitofauti na
zinafanya kazi kwa kushirikiana kulijenga kanisa.
Vivyo
hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni
sana kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa (1Wakoritho 14: 12).
Karama za Roho Mtakatifu hazifanyi kazi kwa ajili ya mtu
binafsi bali kwa ajili ya kulijenga kanisa na si kwa mapenzi ya mtu binafsi
bali kwa mapenzi ya Roho.
“Lakini
kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke
yake kama apendavyo yeye''. (1 Wakoritho 12:11).
Karama za Roho Mtakatifu zimeorodheshwa katika barua ya
kwanza ya mtume Paulo kwa Wakoritho kama inavyosomeka:
Lakini
kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa
neno la hekima na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye
yule; mwingine imani kwa Roho yeye
yule; na mwingine karama za kuponya
katika Ruho yule mmoja; na mwingine matendo
ya miujiza, na mwingine unabii,
na mwingine kupambanua Roho;
mwingine aina za lugha, na mwingine tafsiri za lugha (1Kor 12:7-10).
Orodha nyingine zipo katika: 1Wakoritho 12:26-30; Waefeso
4:11.
7. Hutuzalia matunda ya Roho katika maisha
Haiwezekani kuwa na tunda la Roho kama hatukuwa na Roho
Mtakatifu kwani ndiye hutuletea hayo matunda.
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya
mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja
na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa
Roho, na tuenende kwa Roho (Wagalatia
5:22-25).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni