Yesu kamwambia ndimi njia, na kweli, na uzima,mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi Yohana 14:6
Bwana Yesu Asifiwe Wapendwa.
Namshukuru Mungu kwa wingi wa fadhili zake kwetu.
Mpendwa, yawezekana umekuwa ukiishi bila kutambua
uwezo wa jina la Yesu katika kukuonyesha mwelekeo wa maisha yako.Je, unahitaji mwelekeo mpya katika maisha yako?Je, unahitaji kujua njia ya kutoka katika hali uliyonayo?
Mpendwa , pengine hali ya maisha uliyonayo imekufanya
ukate tamaa na kujiona kwamba hakuna njia ya
kukufanya utimize furaha ya ndoto zako.Je,
unahitaji njia ya kuishi kwa
amani na furaha; njia ya kuwa na
mahusiano mazuri katika ndoa
yako; njia ya kuwa na mahusiano
mazuri na ndugu zako, kazini
kwako, kwenye biashara yako;
unahitaji njia ya kuacha ulevi
wa pombe na madawa ya kulevya, njia ya
kuacha kuabudu sanamu, njia ya
kuacha uongo, njia ya kuacha
uzinzi, njia ya kuacha uchawi,
njia ya kuacha tamaa ya mali
zisizo halali; njia ya kuponywa
maradhi, njia ya kupata utajiri,
njia ya kupata kazi, njia ya
kupata mtaji , njia ya kutoka
kwenye madeni, njia ya kupandishwa
cheo, njia ya kutimiza ndoto
zako?Yesu ni njia ya kila mahitaji yetu hapa duniani, pia yeye ni njia ya kutufanya tujue kweli ya neno lake na tuweze kuurithi uzima wa milele.
Mpendwa, Mungu anatupenda sana; ametupa njia bora kabisa na
anataka tuishi maisha ya ushindi siku zote katika
kila eneo kupitia mwana wake ,Yesu Kristo.Mkaribishe
leo Yesu na mfungulie yote yaliyomo moyoni
mwako ili aweze kukuonyesha njia ya kila
hitaji lako na uakuww na mwelekeo
mpya wa maisha yako.
Neema ya Mungu iwe nanyi
...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni