Sehemu ya Jukwaa litakalotumiwa na Chadema katika
uzinduzi wa kampeni za urais zinazotarajiwa kuzinduliwa katika viwanja
vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo.
Katika uzinduzi huo Chadema kimewataka Watanzania na wananchi
wanaotaka mabadiliko kujitokeza kwa wingi na kumsikiliza mgombea wao
akitangaza mikakati ya ushindi.
Mratibu wa uzinduzi wa kampeni hizo, Deogratias Munishi,
akizungumza na waandishi wa habari jana katika Viwanja vya Jangwani
jijini Dar es Salaam, alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika
kwa asilimia 90.
Uzinduzi huo unafanyika baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
kuruhusu viwanja hivyo kutumiwa cha chama hicho baada ya kuwepo kwa
utata wa kuzuiwa.
Chama hicho ambacho kilipanga kufanya uzinduzi wake Agosti 22,
katika Uwanja Mkuu wa Taifa, kilishindwa baada ya serikali kuzuia
kutumiwa kwa matumizi ya kampeni kwa vyama vyote vya siasa.
WAGENI NCHI MBALIMBALI KUHUDHURIA
Munishi alisema katika uzinduzi huo viongozi na wanachama
mbalimbali kutoka katika matawi ya Chadema nje ya nchi wanatarajiwa
kuhudhuria pamoja na viongozi wote wa Ukawa.
"Tunatarajia kuwa na wageni kutoka nchi ambazo tunawawakilishi
wetu, pia tunatarajia kupokea viongozi na wanachama kutoka mikoa
mbalimbali ikiwamo Arusha, Morogoro na Pwani, "alisema.
Aliwahimiza wananchi wanaoishi jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa
wingi kusikiliza sera za chama na mikakati ya mgombea wa chama hicho
atakayoifanya endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi.
UMEME TANESCO
Aidha, alidai kuwa kama Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
linakusudia kukata umeme siku hiyo, haliwezi kuzuia wananchi kuzifahamu
sera zilizoandaliwa na Ukawa kwa kuwa watazunguka nchi nzima
kuzitangaza.
"Kama Tanesco wanakata umeme hawataweza kuzuia wananchi kusikia
sera nzuri zilizoandaliwa na wagombea wetu kwani tutapita nchi nzima na
tukimaliza uzinduzi ziara ya mikoani zinaanza kesho, "alisema Munishi.
KUANZA ZIARA IRINGA
Akizungumzia ratiba za Mgombea wao wa urais na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, alisema wataanza mikoa ya Iringa na Mtwara.
Munishi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa, alisema Lowassa ataanzia mkoa wa Iringa kwa kufanya
mikutano minne.
"Baada ya kesho (leo), Lowassa keshokutwa (kesho) atakuwa Iringa
katika maeneo manne ya Mufindi, Kilolo, Kalenga na baadae jioni atafanya
mkutano mkubwa wa hadhara Iringa mjini,"alisema.
Alieleza kuwa, Mgombea Mwenza, Duni Haji atakuwa mkoani Mtwara
katika maeneo manne ambayo ni Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na
baadae Mtwara mjini ambako atafanya mkutano mkubwa wa hadhara jioni.
WAJIPANGA KULINDA RAIA
Mbali na Maandalizi hayo, Munishi alisema wamejipanga kulinda
wananchi wote watakaojitokeza kushiriki uzinduzi huo pamoja na mali zao.
Alisema polisi wanataarifa za mkutano wa leo, isipokuwa ni wajibu wao pia kuhakikisha ulinzi na Usalama unakuwepo.
USAFIRI WA ANGA
kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Tumaini Makene, alisema watatumia usafiri waliopanga kwa kufuata
kanuni na taratibu zilizowekwa na nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni