Mojawapo ya mvua kubwa Itwayo El Nino
inatarajiwa kunyesha nchi za Afrika mashariki, ambayo uleta mafuriko na
magonjwa kama maleria.
Hayo yameelezwa wataalumu wa hali ya hewa wa huko kenya , ya kuwa
Mvua hizi ziitwazo El Nino zimeleta wasiwasi mkubwa wa hali ya hewa kwa
1997 watu wengi walipoteza maisha yao na kuacha maelfu ya watu bila
makazi.Wanasayansi wanasema hali hiyo ina uzoefu karibia dunia nzima ambapo inawezekana ikawa ya nguvu kunyesha tangu miaka ya 1950.
Taarifa zinazema, wiki hii Wataalam wa hali ya hewa kutoka nchi za Afrika ya mashariki watakutana mjini Dar es salaam Tanzania kujadili matukio na uwezekano wa kukabiliana na maafa hayo. Vilevile Mashirika ya hali ya hewa duniani kote wamedhitibisha juu ya tukio linaweza kutokea miezi ya hivi karibuni.
Wiki iliyopita Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa Ayub Shaka wa Kenya alisema wakenya wanapaswa kusubiri taarifa zitokazo kwenye mkutano Dar Es Salaam Tanzania juu ya utabiri wa tukio la El Nino, japokuwa utabiri duniani kote unaonyesha uwezekano mkubwa wa El Nino kutokea miezi ijayo hadi mapema 2016.
Na Shirika la Afya Duniani na Shirika la Taassisi ya utafiti wa Hali ya Hewa na Jamii katika Chuo kikuu cha Columbia wantoa onyo juu ya kuzuka kwa malaria kwasababu ya kunyesha mvua nyingi na joto ya hali ya hewa, hata hivyo itabidi kufuatilia mvua hizo zenye mafuriko.
TUJIADHALI
JibuFutaSAWA
Futa